Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndoa hiyo imezuiwa baada ya kuibuka kwa zengwe ambalo wazazi wa Nisha wameshindwa kulielewa.
Zengwe hilo limekuja kufuatia kuibuka kwa mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jennifer ambaye alitumia simu ya mkononi kumchimba mkwara Nisha akimtaka aachane na Kusey kwa sababu ni mume wake.
“Jennifer alimpigia simu Nisha, akamwambia aachane na mumewe ingawa ndoa yao ina migogoro lakini bado ipo hai kwa hiyo hawezi kukubali kuibiwa mume kimachomacho,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta msanii huyo kwa njia ya simu ambapo alikiri kutokea kwa tafrani hiyo na kusema kwamba baada ya tukio hilo aliwataarifu wazazi wake ambao walikataa asiolewe na mwanaume huyo.
Aidha, Nisha alisema miongoni mwa mambo yaliyopingwa na wazazi wake kuhusu Kusey ni pamoja na kumvisha pete ya uchumba baa kitendo ambacho hawakukiafiki kutokana na msimamo wa imani yao ya Dini ya Kiislam.
Akaongeza kuwa wazazi wake wamemtaka mwanaume huyo kusitisha safari yake ya Raha Leo, Zanzibar kwa ajili ya kupeleka barua ya posa.
Msanii huyo alisema amesikitishwa sana na kitendo cha Kusey kumficha ukweli kwamba ni mume wa mtu na alikuwa hajamaliza matatizo na mkewe.
0 comments for "Ndoa ya nisha yapigwa stop"