USIKU wa kuamkia Mei 7, mwaka huu ulikuwa ni wa kizaazaa kwa mastaa wa filamu baada ya majambazi kuvamia katika pub ya Aunt Ezekeil iliyopo Mwananyamala Gereji, jijini Dar kwa lengo la kutaka kupora mali.
Majambazi hao walivamia pub hiyo mishale ya saa sita za usiku, wakiwa na bastola na kufyatua risasi na kusababisha uharibifu mkubwa.
Majambazi hao walivamia pub hiyo mishale ya saa sita za usiku, wakiwa na bastola na kufyatua risasi na kusababisha uharibifu mkubwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo majambazi hao ambao walikuwa wawili walifika katika pub hiyo wakiwa katika pikipiki huku mikononi wakiwa wameshikilia bastola waliwaamuru watu wote kulala chini na kutoa kile walichokuwa nacho.
“Tulisikia, wote laleni chini ole wake atakayeleta ubishi,” alisimulia mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Alisema, walipogundua kuwa watu wote wametii amri yao hiyo ndipo walipoanza kupita meza hadi meza kukusanya simu na kisha kuingia ndani ya pub na kuchukua fedha na vitu mbalimbali.
Alisema, walipogundua kuwa watu wote wametii amri yao hiyo ndipo walipoanza kupita meza hadi meza kukusanya simu na kisha kuingia ndani ya pub na kuchukua fedha na vitu mbalimbali.
Kabla ya majambazi hao hajaondoka rafiki mmoja wa Aunt aitwaye Musa anayeshi Sinza, Dar alionekana kama alitaka kukaidi amri hiyo, ndipo jambazi mmoja akafyatua risasi mbili, moja ikampata mkononi na nyingine mgongoni.
Baada ya kuhakikisha kuwa Musa ametulia baada ya kufyatuliwa risasi hizo, majambazi wale wakawasha pikipiki yao na kutokomea kwa mwendo wa kasi.
Kati ya watu waliokuwepo katika tukio hilo ni msanii maarufu wa filamu nchini, Jacob Steven na Msemaji wa Kampuni ya Usambazaji Filamu ya Steps Entertainment, Selles Mapunda.
“Hakika tumeponea kwenye tundu la sindano, tunashukuru Mungu,” alisema Mapunda.

0 comments for "AUNT AVAMIWA NA MAJAMBAZI"