Latest News!
Advertisement
Related Posts
MIMBA YA LULU YAZUA UTATA 1 Comments
By noe leeTuesday, May 15, 2012 | Posted in
feature
BABA wa marehemu Steven Kanumba, mzee Charles Kusekwa ameufungia kazi ujauzito wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kuibuka na kueleza mkakati utakaomuwezesha kuikomboa damu ya mwanaye.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu juzi, mzee huyo alisema yeye kama baba wa marehemu Kanumba, endapo maelezo ya kwamba Lulu ana ujauzito wa mwanaye yatafikishwa kwake, hawezi ‘kuchomoa’ ila atatumia dawa za kimila ‘DNA ya Kisukuma’ kubaini ukweli.
“Unajua hili suala la ujauzito wa Lulu linazidi kukua kila kukicha sasa mimi nitamaliza ubishi endapo nitakabidhiwa huyo Lulu.
“Nitakachokifanya nitamchukua hadi kijijini kwetu ambapo tutamlisha dawa ya kimila ambayo itatupa ukweli kama hiyo mimba ni ya Kanumba au mtu mwingine, hata kama kaitoa, dawa hiyo itaonesha,” alisema mzee Charles.
Akaongeza kuwa, hata hao wanawake wengine wanaodai kuzaa na mwanaye wamefanya makosa kwenda kumuona mama Kanumba kwani yeye hawezi kujua mambo ya mila za Kisukuma.
“Yule mama Kanumba hawezi kujua mila zetu, wangekuja kwangu wala nisingewakatalia ila ningewapa dawa ambayo naweza kumpa Lulu na ukweli ukajulikana,” alisema.
Lulu ambaye kwa sasa yuko katika Gereza la Segerea jijini Dar akikabiliwa na kesi ya kuhusishwa na kifo cha Kunumba, anadaiwa kuwa na ujauzito wa miezi mitatu huku ukitajwa kuwa ni wa marehemu Kanumba.
Leave a reply
tuone sasa