Latest Stories

Recently Comments


Advertisement

Advertisement
TIGO PATA PATA

News

News

KUTOLEWA KWA JULIO, HILDA BBA... 1 Comments

By noe lee
Wednesday, May 16, 2012 | Posted in


AIBU iliyoje? Tofauti na matarajio ya wengi, Jumapili iliyopita ndani ya Mjengo wa Big Brother Africa (BBA) ‘StarGame’ huko Johannesburg, Afrika Kusini, washiriki watatu walioneshwa mlango wa kutokea wakiwemo Julio Batalia, Hilda (Tanzania) na Teclar (Zimbabwe).
Kutolewa kwa Julio na Hilda kuliongeza machungu kwa Wabongo kwani tukio hilo lilipishana kidogo na lile la Timu ya Soka ya Simba nayo kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.
Mara baada ya tukio hilo, Watanzania wengi walikuwa na maoni tofauti huku lawama nyingi zikimwagwa kwa waliowateua washiriki hao ambao watu wengi hawakuwajua kwani hawakuwa mastaa.
“Hii ni aibu kubwa. Tungempeleka Wema (Sepetu) tusingepata aibu hii kwa sababu anafahamika sehemu kubwa ya Afrika kwa hiyo wangempigia kura abaki mjengoni.
“Tatizo tumepeleka watu ambao siyo mastaa. Hakuna cha kujadili kwani Wabongo tulijua mapema kuwa hatuwezi kufika mbali,” ilisomeka sehemu ya maoni hayo kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.
Hali ilikuwa hivyo hivyo hata katika mitandao mingine ya kijamii kama Twitter na BBM ambapo hoja za wengi ziliegemea kwenye kuwaponda waliotia sahihi Wabongo hao kwenda mjengoni.

ILIKUWAJE?
Alitangulia Julio kuoneshwa mlango wa kutokea na ilipofika zamu ya Hilda ambaye alikuwa kiongozi mjengoni humo wiki iliyopita, alipoambiwa kura hazikutosha hivyo ametolewa, alijikuta akimwaga chozi na kutia huruma lakini akaambiwa kura ndiyo zimemtoa na siyo Biggie.
WABONGO HAWAKUPIGA KURA?
Ilifahamika kuwa siyo kweli kwamba Wabongo hawakupiga kura kwani hata kama wangepiga mamilioni, Julio na Hilda wasingebaki mjengoni.
Utaratibu ni kwamba pamoja na nchi yako kukupigia kura, unatakiwa pia kupigiwa na nchi nyingine tofauti na ilivyokuwa kwa Julio na Hilda hivyo wakaondoshwa ili wakaendelee na mambo mengine ya kujenga taifa.

Follow any responses to the RSS 2.0. Leave a response

Leave a reply

1 comments for "KUTOLEWA KWA JULIO, HILDA BBA..."